JERUSALEM: Mashambulizi ya Israel yaendelea Ukanda wa Gaza
25 Mei 2007Matangazo
Ndege za kivita za Israel zimeendelea kushambulia vituo vya Hamas katika Ukanda wa Gaza.Kwa mujibu wa ripoti ya vyombo vya habari,Wapalestina 4 walijeruhiwa katika mashambulizi hayo.Kwa upande mwingine,wanamgambo wa Kipalestina walivurumisha makombora katika ardhi ya Israel.Ripoti ya jeshi la Israel imesema,makombora hayo yaliangukia kaskazini mwa jangwa la Negev na hakuna aliejeruhiwa.Siku ya Alkhamisi,Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina alitoa wito wa kusitisha mashambulizi ya roketi kutoka Ukanda wa Gaza na kukubaliana na Israel kuweka chini silaha.