1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Mashambulizi ya Israel yaendelea Gaza

26 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBy7

Israel imefanya mashambulio matano ya angani mapema leo asubuhi katika Ukanda wa Gaza.Mashambulizi hayo yalipiga,vituo vya wanamgambo na nyumba ya mlinzi iliyo nje ya nyumba ya Waziri Mkuu wa Wapalestina,Ismail Haniyeh.Na katika shambulio la uvamizi lililofanywa na wanajeshi wa Kiisraeli,wakati wa usiku,kwenye Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, waziri wa nchi Wafsi Qabha alikamatwa nyumbani kwake.Kwa upande mwingine wanamgambo wa Kipalestina wameipa Israel muda wa saa 48 kukubali kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.Mjumbe wa Rais Mahmoud Abbas wa Wapalestina, amesema,makubaliano hayo kwa kweli ni kutekelezwa upya yale makubaliiano ya kusitisha mapigano yaliyotangazwa na Rais Abbas na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert,Novemba iliyopita.Zaidi ya watu 40 wameuawa katika mapigano ya siku kumi zilizopita.