1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Makubaliano ya Rais Katsav yasitishwa

1 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBml

Mahkama Kuu ya Israel imechelewesha kusikiliza makubaliano ya kukiri makosa ya ngono kwa Rais Mosche Katsav na imemtaka mwanasheria mkuu wa Israel ahalalishe kuondelewa kwa mashtaka ya ubakaji kiongozi huyo.

Hatua hiyo inakuja kufuatia shutuma za umma wa wanawake na makundi ya kutetea haki za kiraia pamoja na maandamano ya takriban watu 20,000 mjini Tel Aviv hapo jana.

Mwanasheria Mkuu Menechem Mazuz alikuwa akitazamiwa kuwasilisha makubaliano hayo ya kukiri makosa ya ngono leo hii wakati kujiuzulu kwa Katsav kukianza rasmi.Makundi ya wanawake yameitaka Mahkama Kuu iingile kati makubaliano hayo ambapo kwayo Katsav amekiri makosa madogo madogo ya ngono pamoja na kukubali kutozwa faini.Chini ya makubaliano hayo Katsav aliepushiwa madai mawili ya ubakaji na uwezekano wa kifungo cha gerezani.

Nafasi ya Katsav akiwa rais imepangwa kujazwa na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Shimon Perez.