JERUSALEM: Ehud Barak ashinda duru ya kwanza
29 Mei 2007Matangazo
Waziri Mkuu wa zamani wa Israel,Ehud Barak ameshinda duru ya kwanza ya uchaguzi wa kiongozi wa chama cha Labour.Kiongozi wa hivi sasa wa Labour,Amir Peretz ambae pia ni waziri wa ulinzi wa Israel,ametokea mtu wa tatu katika uchaguzi uliofanywa siku ya Jumatatu.Aliekuwa mkuu wa idara ya usalama wa ndani,Ami Ayalon ameshika nafasi ya pili na atapambana na Barak katika duru ya pili,baada ya majuma mawili.Chama cha Labour ni mshirika katika serikali ya mseto ya Waziri Mkuu Ehud Olmert.