JENIN : Wanajeshi wa Israel wauwa Wapalestina wawili | Habari za Ulimwengu | DW | 27.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JENIN : Wanajeshi wa Israel wauwa Wapalestina wawili

Wanajeshi wa Israel wamewauwa Wapalestina wawili akiwemo mwanamke mkongwe karibu na mji wa Ukingo wa Magharibi wa Jenin.

Kwa mujibu wa duru za hospitali za Palestina mauaji hayo yametokea leo hii katika mashambuliano ya risasi wakati wanajeshi wa Israel walipouvamia mji wa Qabatia kusini ya Jenin wakiwasaka wanamgambo.Mauaji hayo yanadhoofisha suluhu ilio tete iliotangazwa hapo jana wakati makundi ya Kipalestina yakidai Israel isitishe mashambulizi yake katika ardhi za Wapalestina.

Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema anataraji suluhu hiyo ya kusitisha mapigano inaweza pia kutumika kwenye Ukingo wa Magharibi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com