1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jean-François M Gisimba LONDON: Matajiri wanaomiliki viwanda kutoka nchi washirika wa Marekani, wakutana London-

21 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFzF
Matajiri zaidi ya miambili hamsini, kutoka nchi washirika wa Marekani katika vita vyake nchini Irak, leo wamekua na mkutano ulioandaliwa kwa siri, katika mji mkuu wa Uingereza London. Duru rasmi mjini London, zimearifu mkutano huo umeandaliwa na wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon, na ulilenga kujadiliana juu ya ujenzi mpya wa Irak. Msemaji wa taasisi ya serikali ya Uingereza ya biashara na uchukuzi, amewaambia waandishi wa habari, kwamba waliohudhuria mkutano wa leo mjini London, walifahamishwa utaratibu mpya wa kupata mikataba ya ujenzi wa miradi tofauti nchini Irak, utaratibu ambao unayafungulia milango zaidi kuliko ilivokua awali, mashirika yasiyokuwa ya kimarekani. Akasema kitita cha dola za kimarekani zaidi ya biliyoni kumi na nane, kimetengwa na serikali ya Marekani, kwa ajili ya miradi ya ujenzi nchini Irak.