Je, Zanzibar ni Nchi?
14 Julai 2008Matangazo
Yaonesha viongozi wa Chama cha Mapinduzi huko Zanzibar na pia wa chamna cha upinzani cha CUF wana msimamo mmoja kupinga tamko hilo la Bwana Pinda. Chama cha CUF kimewahimiza viongozi wa CCM wa Zanzibar watangaze mzozo wa kikatiba kutokana na tamko la Mizengo Pinda. Halima Nyanza alizungumza kwa njia ya simu na makamo wa katibu mkuu wa Chama cha CUF, upande wa Zanzibar, Juma Duni, na alielezea hivi namna chama chake kinavoyaona mabishano haya: