1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, ni nini maana ya upotoshaji kuhusu tabia nchi?

John Juma Martin Kuebler
29 Januari 2024

Upotoshaji ni pale watu wanapoeneza habari ya uwongo kuhusu utoaji gesi chafu kutokana na nishati ya visukuku au taarifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, isiyoleta taswira kamili na inayoweza kushawishi fikra za watu.

https://p.dw.com/p/4bn2z
Barabara zilizojaa maji mjini Katesh, Tanzania.
Barabara zilizojaa maji mjini Katesh, Tanzania.Picha: Uncredited/AP Photo/picture alliance

Si lazima iwe kwa makusudi. Baadhi ya habari potofu huweza kutokana na makosa madogo, au kutoelewa suala zima.

Kwa mfano matangazo ambayo mashirika hueneza yakizipa bidhaa zao sifa kedekede kwamba zinajali na kukidhi hali ya usalama wa mazingira. Lakini ukweli ni kwamba sifa wanazozungumzia ni kinyume na hali halisi.

Baadhi ya kampuni za nguo hunadi bidhaa zao kuwa zimetengenezwa kwa nyuzi asilia, kwamba zinaweza kutumika tena.

Soma pia: COP28 yafikia makubaliano kuachana na nishati za visukuku

Kwa upande mwingine, upotoshaji ni pale wanaopinga masuala ya tabia nchi yakiwemo baadhi ya makundi au mashirika rasmi, huamua kusambaza taarifa za kupotosha kwa makusudi ili kuendeleza ajenda zao dhidi ya sayansi kuhusu tabia nchi na sera za serikali zinazolenga kufaidi mazingira.

Je, ni vipi upotoshaji huathiri juhudi za kukabili mabadiliko ya tabia nchi?

Maandamano ya kushinikiza kukomesha matumizi ya mafuta ya visukuku
Maandamano ya kushinikiza kukomesha matumizi ya mafuta ya visukukuPicha: Peter Dejong/AP Photo/picture alliance

Kampuni kubwa za mafuta kama Shell, Exxon Mobil, BP, muungano wa wapinzani wa tabia nchi, na kundi la kampuni za mafuta zilizovunjwa mnamo mwaka 2002, zimeshutumiwa kwa kudharau sayansi ya hali ya hewa au kuficha uwekezaji wao katika sekta ya mafuta na kushawishi watu kutumia matangazo ya kuwarai watu tangu mwishoni mwa miaka ya 1970.

Mashirika kama The Empowerment Alliance ya Marekani au Responsible Energy Citizen Coalition la Ulaya, kwa mfano hutumia mbinu ya kuwaficha wafadhili wao. Hivyo kudai kuwa kama vuguvugu la watu wa kawaida - kusaidia gesi asilia inayotokana na nishati ya visukuku na kudharau sera salama. Mara nyingi kwa ufadhili kutoka kwa vyanzo visivyoeleweka.

Habari potofu na uwongo pia huchapishwa na baadhi ya vyombo vya habari, au kusambazwa na wanasiasa wanaopenda umaarufu.

Soma pia: Mazungumzo ya COP28 kuamua juu ya nishati ya kisukuku?

Wakati kimbunga kiliposababisha mafuriko na kuua zaidi ya watu 40 nchini Brazil mnamo Septemba mwaka 2023, wapinzani wa serikali na baadhi ya waandishi habari mashuhuri walilaumu vifo hivyo kusababishwa na bwawa lililoharibika. Ikiwa ni jaribio la kubadili fikra za watu kutoka kwa juhudi za kupunguza athari mbaya za joto ulimwenguni.

Upotoshaji kuhusu tabia nchi hushuhudiwa pia kwenye mitandao ya kijamii ambapo picha au video bandia husambazwa, hasa inapohusishwa na nadharia za njama, kama vile chuki ya hivi karibuni dhidi ya mwelekeo endelevu wa mipango ya miji ya dakika 15.

Je, ni kwa nini ni muhimu kuwa makini kuweza kubaini taarifa potofu ya hali ya hewa?

Moshi ukifuka kutoka kiwanda cha chuma Inner Mongolia, China.
Moshi ukifuka kutoka kiwanda cha chuma Inner Mongolia, China.Picha: Kevin Frayer/Getty Images

Kadri utoaji gesi chafuzi na hali ya joto duniani zikikaribia rekodi moja zaidi baada ya nyingine, ndivyo muda wa kushughulikia tatizo la ongezeko la joto duniani unavyozidi kuyoyoma.

Wanasayansi wengi wanaamini kwamba tunahitaji kuchukua hatua sasa. Lakini upotoshaji unasababisha watu kuhoji sayansi ya hali ya hewa iliyothibitishwa kwamba ubinadamu umesababisha mabadiliko ya hali ya hewa,na kutilia shaka suluhisho, hali inayodhoofisha msaada wa umma kwwenye mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Soma pia: COP28: Ahadi za kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi hazitekelezwi ipasavyo 

Vikundi vya utetezi kama vile Hatua ya Hali ya Hewa Dhidi ya upotoshaji, serikali, Umoja wa Ulaya na mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, Shirika la Hali ya Hewa Duniani na Shirika la Afya Ulimwenguni, miongoni mwa mengine, yanajitahidi kutoa wito na kukabiliana na taarifa potofu.

Aidha, mashirika mengi ya habari pia yamejitolea kuripoti masuala ya hali ya hewa na kuondoa taarifa za udanganyifu wa kimazingira.