Jaribio jengine la kombora lenye nguvu za kinuklea la Pakistan | Habari za Ulimwengu | DW | 16.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Jaribio jengine la kombora lenye nguvu za kinuklea la Pakistan

Islamabad:

Pakistan imefanya jaribio jengine la kombora la masafa ya wastani siku moja tuu baada ya duru mpya ya mazungumzo ya amani pamoja na India.Msemaji wa kijeshi amesema mjini Islamabad jaribio hilo limefanikiwa..India na nchi nyengine jirani ziliarifiwa kabla ya hapo,msemaji huyo ameshadidia.Kombora hilo chapa Hatf nambari 5 lina uwezo wa kupiga hadi umbali wa kilomita 1300.India na pakistan zimekua kila kwa mara zikifanya maajaribio ya makombora yao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com