1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Janga la moto nchini Kenya,serikali yatangaza maombolezo ya kitaifa

Abdu Said Mtullya14 Septemba 2011

Waliokufa kutokana na maafa ya moto sasa wafikia 87.

https://p.dw.com/p/12Yjz

Nchini Kenya idadi ya watu waliokufa kutokana na mripuko wa bomba la mafuta imeongezaka na kufikia 87.

Mratibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Pamela Indiaka amearifu kwamba watu watano zaidi wamekufa hospitalini wakati wakitibiwa majeraha yaliyotokana na kuungua sana.

Kutokana na maafa hayo serikali ya Kenya imetangaza maombolezo ya kitaifa kwa muda wa siku mbili.

Serikali ya Kenya pia imeahidi kuwasaidia wahanga kifedha.

Maafa hayo ya moto yalitokea juzi kwenye mtaa wa mabanda katika kitongoji kimoja cha Nairobi.