1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jamhuri ya Afrika Kati

21 Februari 2007

Jamhuri ya Afrika ya Kati ni nchi isiotambulikana duniani.Umasikini umezagaa licha ya madini ilizonazo.Usafiri ni taabu na kuna upungufu wa kila kitu nchini.Nchi ya aliekua mfalme "Bokassa" ihali gani leo ?

https://p.dw.com/p/CHJg

“Kuna upungufu humu nchini wa kila kitu.Jamhuri ya Afrika ya kati ni nchi gain hii ? Inakutikana wapi ?”-aliuliza mtumishi mmoja wa shughuli za misaada.

Mahala ilipo nchi hii ndio neema yake na bkuapizwa kwake:Wafaransa waliliita koloni lao la zamani Oubangui-Chari ikitumia jina löa mito ipitayo mpakani mwake kusini na kaskazini.Baadae nchi hii ikachukua jina la “Jamhuri ya Afrika Kati”-Republique CentralAfricaine- ilipokua inaelekea uhuru 1960.

“Jamhuri ya Afrika ya kati iko mahala muhimu kijiografia na sio kwa kuwa ina nguvu,lakini kwa kuwa ina majirani wenye nguvu.”-alisema mchunguzi mmmoja katika mji mkuu Bangui.

Katika eneo masikini,majirani kama vile Kamerun,Chad,Sudan,Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo zote zina ushawishi mkubwa kisiasa kwa nchi hii lakini pia kutokana na utajiri wao wa mali asili.

Waasi wa Kongo na wa Chad waliingia Jamhuri ya Afrika kati kupora mali nyakati za miaka ya mapinduzi ya kijeshi na machafuko chini ya utawala wa jamadari Jean-Bedel Bokassa,aliejuitawaza binafsi mfalme katika sherehe nono kabisa na kiongozi ambae akisemekana ni mla watu.

Mwaka jana serikali ya bangui iliituhumu Sudan kuwasaidia waasi walionyakua eneo dogo la kaskazini-mashariki kandoni mwa Birao kabla kutimuliwa na na vikosi maalumu vya Ufaransa vilivyosaidiwa na ndege za helikopta na za kivita.

Rais Francois Bozize amegundua kwamba wengi wa wajumbe wake na maafisa hawakuwahi hata kutembelea mji huo wa Birao uliopo masafa ya masaa 3 tu kutoka mji mkuu bangui kwa ndege au kwa gari.

Mahala ilipo JYAK katika ramani inaiumiza mno kiuchumi nchi hii kwavile sehemu kubwa ya bidhaa zake inayoagiza na inayosafirisha n’gambo kubidi kupitia barabara km 1,450 kutoka Bangui-mji mkuu hadi Douala, bandari ya Kamerun katika bahari ya Atlantik.Hii kwa muujibu wa uchunguzi safari hiyo hudumu hadi mwezi pamoja na ucheleweshaji wa idara za forodha.

Kwahivyo, wanabiashara wanaosafirisha n’gambo bidhaa zao na wale wanaoagiza kutoka n’gambo bidhaa wanabeba gharama kubwa kabisa ya usafiri wa barabarani duniani.

Pamba mojawapo ya bidhaa kubwa inazosafirisha nje Jamhuri hii hugharimu hadi faranga 120,000 kwa tani moja kuisafirisha hadi bandari ya Duala,nchini Kamerun.

Kwa sasa serikali ya Bangui, imenin’giniza matarajio yake juu ya mali-asili dhahabu kukuza uchumi wake,lakini pia almasi,uranium na madini nyenginezo.Hatahivyo, hakuna miradi ya kutosha ya kuchimba madini hizo kibiashara.

Njia nyengine ya kusafirisha shehena mbali na hiyo ya Duala, inapitia bandari ya pointe Noire,nchini Kongo-Brazzaville kupitia mtoni.

Waziri mkuu Elie Dote amesema serikali yake inasaka njia nyengine za usafiri kupitia Gabon au hata port Sudan.

Kwahivyo, umasikini,machafuko na maradhi ya UKIMWI yaliofikia kipimo cha 15% miongoni mwa wakaazi wake,kumeongoza katika vifo vya watoto wadogo kupanda kwa zaidi ya mtoto 1 katika 5 na matarajio ya kuishi kwa wakaazi wake Jamhuri ya afrika ya Kati yamepungua kwa miaka 5 na kuwa umri wa miaka 38.

“Jamhuri ya Afrika ya kati haina sauti ulimwenguni”-alinukuliwa mtumishi mmoja wa misaada kutoka nje akisema.