1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

James Jones ateuliwa mjumbe mpya wa Marekani katika Mashariki ya Kati

29 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUPO

Rais George W Bush wa Marekani amemteua kamanda wa zamani wa jumuiya ya kujihami ya kambi ya magharibi, NATO, jenerali James Jones, kuwa mjumbe mpya wa Marekani atakayeushughulikia mpango wa amani wa Mashariki ya Kati unaohusu kuundwa kwa taifa huru la Palestina.

Tangazo hilo limetolewa mda mfupi baada ya rais Bush kukutana na waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert, na rais wa mamlaka ya ndani ya Wapalesrina, Mahmoud Abbas, katika ikulu ya Marekani mjini Washington.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amesema njia pekee itakayosaidia kuundwa kwa taifa huru la Palestina ni kuhakikisha kuna amani Mashariki ya Kati na mtu anayefaa kuongoza juhudi hizo ni jenerali James Jones.

Rais Bush ameahidi Marekani itajitolea kwa dhati kusaidia juhudi za kuyafikia makubaliano ya amani ya Mashariki ya Kati.