1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA : Msako waimarishwa kutafuta ndege iliopotea

7 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcd

Indonesia imeimarisha msako wake wa ndege ya abiria iliokuwa na watu 102 ambayo ilitoweka kutokana na hali mbaya ya hewa takriban wiki moja iliopita.

Wanajeshi 700 na helikopta nne zaidi zitaongezwa kwenye msako huo wa ndege hiyo ya Indonesia aina ya Boeing 737 ilioundwa miaka 17 iliopita.

Karibu wanajeshi na polisi 2,000 wa Indonesia na ndege za nne za kijeshi wamekuwa wakiitafuta ndege hiyo iliopotea.

Msako huo awali ulikuwa umelenga kwenye maeneo ya magharibi mwa Sulawesi ambapo ishara ya mwisho ya hadhari ilipokelewa kutoka kwenye ndege hiyo lakini hapo Ijumaa umetanuliwa kwa kuyajumuisha maeneo ya kaskazini na mashariki ya kisiwa hicho.