JAKARTA : Mafuriko ya Asia yauwa watu 70 | Habari za Ulimwengu | DW | 25.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JAKARTA : Mafuriko ya Asia yauwa watu 70

Takriban watu 70 wamekufa na wengine 200,000 wamelazimia kukimbia makaazi yao kutokana na mafuriko ambayo yamekumba sehemu fulani za Indonesia na Malaysia katika kipindi cha wiki moja iliopita.

Nchini Indonesia waokozi wamegunduwa maiti 60 hapo jana lakini mamia ya watu bado hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kunyesha kwenye kisiwa cha Sumatra.Shirika la habari la taifa Antara limeripoti kwamba watu 114 wameuwawa kutokana na mafuriko hayo.

Umoja wa Mataifa umesema utatowa dola milioni mbili ikiwa ni sehemu ya kwanza ya msaada wa dharura kwa jimbo la Aceh kutokana na watu 110,000 kupoteza makaazi yao katika jimbo hilo ambalo liliathiriwa vibaya na gharika la Tsnunami hapo mwaka 2004.

Nchini Malaysia maafisa wanasema watu saba wameuwawa na wengine karibu 90,000 wamelazimika kuzihama nyumba zao katika mafuriko mabaya kabisa kuwahi kuikumba nchi hiyo kwa miongo kadhaa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com