JAKARTA: Homa ya mafua ya ndege yazuka tena | Habari za Ulimwengu | DW | 12.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JAKARTA: Homa ya mafua ya ndege yazuka tena

Homa ya mafua ya ndege imetokea tena nchini Indonesia huku mtu wa pili akiripotiwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

Maofisa wamesema mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 37 amefariki dunia katika hospitali moja mjini Jakarta wiki mbili baada ya kula nyama ya kuku aliyekuwa akiugua homa ya mafua ya ndege. Mwanamke huyo ni mtu wa 59 duniani kufariki kutokana na ugonjwa huo.

Nchini Vietnam virusi vinavyosababisha ugonjwa huo aina ya H5 N1 vimeshambulia ndege kwenye mashamba yaliyo karibu na maeneo ya mji wa Ho Chi Mihn.

Japan pia inakabiliwa na hatari ya kuzuka ugonjwa wa homa ya mafua ya ndege katika kisiwa chake cha Kyushu kusini mwa nchi hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 2004.

Mamia ya kuku wamekufa mjini Miyazaki katika kipindi cha siku chache. Wizara ya kilimo inasubiri matokeo ya uchunguzi wa mahabara kubainisha ikiwa virusi vya H5 N1 vilisababisha vifo vya kuku hao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com