JAKARTA: Abiria takriban 90 wauwawa katika ajali ya ndege | Habari za Ulimwengu | DW | 02.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JAKARTA: Abiria takriban 90 wauwawa katika ajali ya ndege

Abiria wasiopungua 90 wamekufa baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuanguka katika eneo la milimani katika kisiwa cha Sulawesi nchini Indonesia kufuatia hali mbaya ya hewa. Hatima ya abiria wengine 12 haijulikani.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737-400 ya shirika la ndege la Adam Air iliashiria ilikuwa katika matatizo kabla kupoteza mawasiliano na maofisa wanaoongoza safari za ndege. Juhudi za kuitafuta ndege hiyo zilitatizwa kwa sababu ya hali mbaya ya hewa.

Ndege hiyo ilikaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Manado Sulawesi Kaskazini ikitokea Surabaya kisiwani Java.

Wakati haya yakiarifiwa, maofisa wa uokozi nchini Indonesia wamefaulu kuwaokoa watu takriban 191 wakiwa wazima kufuatia kuzama kwa feri katika pwani ya kisiwa cha Java Ijumaa wiki iliyopita. Mpaka sasa watu zaidi ya 400 hawajulikani waliko.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com