Jaji Mkuu wa Pakistan amerejea kazini
21 Julai 2007Matangazo
Mahakama Kuu ya Pakistan,imeamua kuwa hatua iliyochukuliwa na Rais Musharraf tarehe 9 mwezi wa Machi,kumfukuza kazi jaji mkuu Chaudhry,si halali.Umamuzi wa Mahakama Kuu unatazamwa kama ni pigo kwa Musharraf na mamlaka yake.
Lakini Naibu-Waziri wa habari wa Pakistan,Tariq Azim Khan ana maoni mengine.Alipohojiwa na CNN,Khan alisema,huenda ikawa nafasi ya Rais Musharraf imeimarishwa.Akaeleza kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya Pakistan,serikali haikuwashinikiza majaji na waliachiwa uhuru wa kuitafsiri katiba kama ipasavyo kutafsiriwa.