1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

J3 0809 News

8 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRo

Modena , Italia . Pavarotti azikwa.

Mamia ya waombolezaji wakiongozwa na viongozi wa ngazi ya juu wa kisiasa na nyota wa masuala ya burudani wamehudhuria mazishi ya mtoaburudani mashuhuri katika muziki wa Opera Luciano Pavarotti.

Misa kwa ajili ya mwimbaji huyo wa Opera , ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 71 , ilifanyika katika kanisa Katoliki katika mji alikozaliwa Pavarotti wa Modena.

Kiasi cha marafiki wa familia yake watapa 800 na wageni mashuhuri ikiwa ni pamoja na katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Kofi Annan na waziri mkuu wa Italia Romano Prodi , mtaarishaji mwongozaji wa filamu nchini Italia Franco Zeffirelli pamoja na mwimbaji mashuhuri wa muziki wa Rock Bono ni baadhi ya watu mashuhuri waliohudhuria mazishi hayo.Mamia kadha ya watu wengine waliangalia mazishi hayo kupitia luninga kubwa zilizotundikwa nje ya kanisa hilo.