1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

J3 0809 News

8 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRn

Vienna. Benedict 16 azuru Austria.

Kiongozi wa kanisa katoliki Pope Bebedikt wa 16 amezuru katika eneo maarufu la ibada la bikira Maria nchini Austria.

Ameanza hivi sasa kuendesha misa ya wazi katika eneo la Mariazell.

Eneo hilo liko kilometa 150 kusini magharibi ya mji mkuu wa Austria wa Vienna.

Kiasi cha waumini 30,000 wanatarajiwa kuhudhuria tukio hilo, ambalo lilipangwa kuadhimisha mwaka wa 850 wa eneo hilo la ibada.

Hii ni siku ya pili ya ziara ya siku tatu ya Papa nchini Australia. Jana Ijumaa alizuru eneo la makumbusho ya mauaji ya halaiki ya Holocaust, mjini Vienna, na kukutana na rais wa nchi hiyo Heinz Fischer.