Ivory Coast
27 Novemba 2010Wapinzani wakisiasa nchini Ivory Coast hapo jana walikamilisha mikutano ya kampeni za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hapo kesho na ambao unatarajiwa kumaliza mwongo mmoja wa kutoimarika kwa nchi hiyo inayogubikwa na hofu na umwagikaji damu.
Maelfu ya wafuasi walimiminika katika mikutano tofauti ya rais Laurent Gbabo na mpinzani wake Alassane Outtara katika mji mkuu wa kibiashara wa Abidjan, ambao ni eneo kuu la upigaji kura katika nchi hiyo iliyogawanyika.
Wagombea wa uchaguzi huo wametoa wito wa kupigwa kura kwa amani, lakini dalili za vurugu zilionekana wakati kambi ya Outtara ilipokataa wito wa Gbabo wa kuwepo amri ya kutotembea baada ya uchaguzi wa kesho. Vikosi vya jeshi nchini humo na vya Umoja wa Mataifa vimemiminika kuimarisha usalama iwapo patazuka vurugu.
Mwandishi :Maryam Abdalla/Afpe
Mhariri:Sekione Kitojo