ISTANBUL: Polisi wa Uturuki wamkamata mshukiwa wa mauaji ya Hrant Dink. | Habari za Ulimwengu | DW | 21.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISTANBUL: Polisi wa Uturuki wamkamata mshukiwa wa mauaji ya Hrant Dink.

Polisi wa Uturuki wamemkamata mshukiwa wa mauaji ya mwandishi wa habari mturuki Hrant Dink mwenye asili ya Kiarmenia.

Maafisa wanasema mshukiwa huyo alikamatwa ndani ya basi katika mji wa kitalii wa Samsun.

Hrant Dink mwenye umri wa miaka hamsini na mitatu aliuawa kwa kupigwa risasi nje ya afisi za Istanbul za gazeti lake la Agos.

Wazalendo wa Kituruki walikasirishwa na maelezo aliyotoa Hrant Dink kuhusu mauaji ya jumla jamala ya Warmenia nchini Uturuki kati ya mwaka elfu moja mia tisa na kumi na tano na mwaka elfu moja mia tisa na kumi na nane.

Kwenye makala yake ya mwisho aliyoandika, mwandishi huyo wa habari alieleza alikuwa amepata vitisho vya kuuawa kutoka kwa wazalendo hao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com