Istanbul. Mwanajeshi wa Uturuki auwawa. | Habari za Ulimwengu | DW | 08.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Istanbul. Mwanajeshi wa Uturuki auwawa.

Mwanajeshi mmoja wa Uturuki ameuwawa na wengine watatu wamejeruhiwa katika mlipuko wa bomu lililotegwa ardhini katika jimbo la kusini mashariki la Diyarbakir.

Hii inakuja siku moja baada ya waasi wa Kikurdi kutoka katika kundi la PKK, kuwauwa wanajeshi 13 katika moja ya hasara kubwa zilizolikumba jeshi la Uturuki katika mapigano na kundi hilo.

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameshutumu shambulio hilo, akisema kuwa mapambano ya nchi yake dhidi ya magaidi yatachukua mtazamo mwingine kabisa. Jeshi la Uturuki limekuwa kwa miezi kadha likitaka kufanya mashambulio ndani ya eneo la kaskazini mwa Iraq ambako wapiganaji wa PKK wana ngome yao. Jopo linalopambana na ugaidi nchini Uturuki litakutana leo Jumatatu kujadili suala hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com