1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL: Mauaji ya mwandishi wa habari Hrant Dink yalaaniwa.

20 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZQ
Balozi wa Marekani katika Iraq, Ryan Crocker
Balozi wa Marekani katika Iraq, Ryan CrockerPicha: AP

Mauaji ya mwandishi wa habari mturuki Hrant Dink mwenye asili ya Armenia yameshutumiwa na watu na makundi mbali mbali kote duniani.

Mwandishi huyo wa habari alipigwa risasi na kuuawa nje ya afisi ya gazeti alilokuwa akifanyia kazi

Hrant Dink aliingia matatani kwanza kwa maoni yake yaliyozua hasira kuhusu mauaji ya raia wa Kiarmenia waliouawa kati ya mwaka elfu moja mia tisa na kumi na tano na mwaka elfu moja mia tisa na kumi na nane nchini Uturuki.

Mwaka uliopita Hirant Dink alihukumiwa kifungo cha miezi sita kwa kuvunja sheria kwa kutoa matamshi yaliyosemekana yalidharau utaifa wa Uturuki.

Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan ameshutumu waliomuua mwandishi huyo wa habari akisema kitendo hicho ni sawa na kutatiza uhuru wa kutoa maoni.

Waandishi wa habari na wanasiasa nchini Uturuki wameelezea kufadhaishwa na mauaji hayo ambayo wengine wao wamedai ni ya kisiasa.

Makundi kadha ya kutetea haki za binadamu, Marekani, Umoja wa Ulaya na Armenia zimeshutumu wauaji wa mwandishi huyo wa habari.