1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yazidisha mashambulizi Gaza

20 Novemba 2023

Gaza huenda ikakabiliwa na operesheni kubwa zaidi kutoka Israel licha ya matumaini ya kufikiwa kwa makubaliano ya kuwaachia watu waliochukuliwa mateka na kundi la Hamas ili mapigano yasitishwa kwa muda.

https://p.dw.com/p/4ZAtl
Wanajeshi wa Israel wakiwa na zana za kivita wakishambulia Gaza
Wanajeshi wa Israel wakiwa na zana za kivita wakishambulia GazaPicha: Israel Defense Forces/Handout/REUTERS

Kulingana na serikali inayoendeshwa na Hamas upande wa Gaza, Jeshi la Israel limesema linaelekeza vita vyake dhidi ya kundi hilo katika maeneo jirani ya Gaza  ambako operesheni za angani na ardhini tayari zimesababisha mauaji ya watu 13,000 wakiwemo maelfu ya watoto.

Soma pia:Israel yazidisha mashambulizi ya mabomu dhidi ya Gaza

Wapatanishi wa Qatar walisema jana kwamba mazungumzo ya kuwaachia huru mateka yanaendelea vizuri na yanakwamishwa tu na mambo madogo bila ya kutoa taarifa zaidi na muda hasa wa hicho kufanyika. Israel na Hamas pia hawajatoa taarifa zaidi juu ya mpango huo.