Israel yasema wakati umefika kufikiria juu ya Ukanda wa Gaza.
16 Juni 2010Matangazo
Kutokana na ongezeko la shinikizo la kimataifa Israel sasa inafikiria kulegeza masharti ya kuifunga mipaka ya Ukanda wa Gaza.
Msemaji wa serikali ya Israel amefahamisha kwamba waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ,leo atakutana na baraza lake la mawaziri , kujadili juu ya kuirefusha orodha ya mahitaji yanayoweza kuruhusiwa kuingizwa katika Ukanda wa Gaza- sehemu inayodhibitwa na Hamas.
Waziri wa masuala ya kijamii Isaac Herzog amesema wakati sasa umefika wa kubadili namna ambayvo mipaka ya Ukanda wa Gaza imekuwa inafungwa.
Lakini Israel wakati wote imekuwa inahoji kwamba imeifunga mipaka ya Ukanda wa Gaza ili kuzuia silaha kupenyezwa kwa ajili ya Hamas.