Israel yaikamata meli nyingine ya misaada
5 Juni 2010Israel inameikamata meli nyingine ya misaada iliyokuwa inaelekea Gaza, hatua inayozidisha wasiwasi zaidi kuhusiana na hatua ya Israel kulizingira eneo la Gaza linalotawaliwa na kundi la Hamas. Israel imekabiliwa na shutma za kimataifa baada ya operesheni yake ya Jumatatu, pale wanaharakati tisa wa Uturuki walipouawa ndani ya meli iliyokuwa inaelekea Gaza. Israel imesisitiza uamuzi wake wa kuendelea kulizingira kijeshi eneo la Gaza, baada ya kundi la Hamas kuchukua mamlaka, ni kuzuwia kuingizwa kwa silaha. Mjini Washington, Ikulu ya Marekani imesema hatua ya Israel kulizingira eneo la Gaza haina maana ya kuendelezwa lakini, pia Ikulu hiyo ikazihimiza meli za misaada zinazoelekea Gaza kuelekea katika bandari ya Israel ili kuzuia kutokea kwa rabsha.