1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Israel na Hamas kuendelea kubadilishana wafungwa na mateka

25 Novemba 2023

Mpango wa muda wa usitishwaji mapigano huko Gaza kati ya Israel na kundi la Hamas umeingia katika siku yake ya pili hii leo.

https://p.dw.com/p/4ZREp
Westjordanland | Ehemalige palästinensische Gefangene, die von den israelischen Behörden freigelassen wurden
Waliokuwa wafungwa wa Kipalestina walioachiwa na Israel wakiwa na bendera ya Palestina na Hamas:24.11.2023Picha: Nasser Nasser/AP/picture alliance

Pande hizo mbili zinatarajia pia kuendelea na zoezi la kubadilishana wafungwa na mateka. Israel imesema imepokea orodha ya kundi la pili la mateka watakaoachiliwa.

Katika siku hizo nne za makubaliano hayo, Hamas itawaachilia mateka wasiopungua 50 kati ya 240 inaowashikilia,  huku Israel ikiwaachia wafungwa wapatao 150 wa Kipalestina.

Soma pia: Israel na Hamas wabadilishana mateka, wafungwa

Hayo yakiarifiwa, Shirika la Afya Duniani WHO limesema lilifanikiwa Novemba 22, kuwahamisha wagonjwa zaidi ya 150, jamaa zao pamoja na wahudumu wa afya kutoka hospitali ya Al-Shifa huko Gaza, na wamesema ilikuwa operesheni hatari kwani ilikuwa kabla ya mpango huu wa usitishwaji mapigano.