Israel inataka kuirejesha milima ya Golan kwa nchi ya Syria | Matukio ya Kisiasa | DW | 08.06.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Israel inataka kuirejesha milima ya Golan kwa nchi ya Syria

Gazeti maaruf la Israel, Yediot Aharonot, limesema waziri mkuu wa Israel sasa anaonekana huenda akaridhia matakwa ya nchi ya Syria, kuirejeshea milima ya Golan, Israel ilioiteka mwaka wa 67.

Eneo la mlima wa Golan

Eneo la mlima wa Golan

Waziri mkuu wa Israel ameitaka Syria kwanza iwachane na vitendo vya kigaidi na pia ikomesha kuyasaidia makundi ya wapiganaji wa kipalastina na Hezbullah, ndipo Amani ya kweli itapatikana.

Gazeti maaruf nchini Israel la Yediot Aharonot, leo limesema waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amekua akituma ujumbe wa siri kwa kiongozi wa Syria ,Bashar Al –Assad ili akimueleza kua Israel iko tayari kuirejeshea Syria eneo la milima ya Golan, Israel ilioiteka katika vita vya mwaka 1967.

Repoti hio ya Gazeti la Aharonot inaendelea kusema,ujumbe wa waziri mkuu, Ehud Olmert kwa Rais Bashar Al –Assad umekua ukipitia nchi ya Ujerumani na Uturuki, kwa njia za Kideplomasia Kua Amani ya kweli itapatikana baina ya nchi mbili hizo, ikiwa Syria itakubali kuvunja uhusiano wake na nchi ya Iran, kukomesha kugharimia makundi ya kigaidi yanayoipiga vita Israel mfano kundi la Hezbullah,na makundi mengineyo ya kipalastina mkiwemo kundi la Hamas kiongozi wake akiishi uhamishoni nchini Syria.

Inasemekana Bw Olmert amechukua uamuzi huo baada ya kuzungumza na Rais George Bush wa US na kumkubalia afanye hivo.

Msemaji wa waziri mkuu wa Israel , Yanki Galanti hajakubali au kukanusha habari hizo.

Lakini waziri wa Biashara na viwanda wa Israel, Eli Yishai akizungumza leo na Redio ya Serekali, amesema yeye yuko tayari kukubali mpango huo wa kubadilishiana Ardhi kwa Amani, ili kunusuru maisha ya Raia wa Israel.

Pia waziri Eli amemsihi Rais Bashar El-Assad aizuru Jerusalem kwa mpango huo wa amani kama alivofanya Rais wa Misri Marhemu Anwar Sadat ambae mwaka 1979 Israel ilisaini mkataba wa Amani na Misri na kuirejeshea Misri eneo la Sinai. Lakini baadae waislamu wenye itikadi kali walimuua Rais Sadat kwa uamuzi wake wa kukubaliana na Israel.

Kwa upande wao, viongozi wa Syria wamesema, Damascus iko tayari kwa mazungumzo na Israel lakini hawaoni kama Israel ina imani ya kweli ya kufanya mazungumzo ya Amani.

Kura ya maoni iliopigwa na gazeti la Maariv la Israel, imeonyesha ni 10% tu ya waisrael wanaopendelea Israel itoke kwenye milima ya Golan .

Mbunge wa mrengo wa kulia Gideon Saar, wa chama cha Likud amesema, wananchi wa Israel hawakubaliani na waziri mkuu Ehud Olmert katika suala hilo, na utawala wake ni tishio kwa usalama wa Israel,ikiwa Bw Olmert ataendelea na mpango huo.

 • Tarehe 08.06.2007
 • Mwandishi Omar Mutasa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHCx
 • Tarehe 08.06.2007
 • Mwandishi Omar Mutasa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHCx

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com