1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISMAILIA:Raia wa Msiri apiga mbizi usiku kucha

26 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVm

Mwanamume mmoja wa Misri amepiga mbizi usiku kucha kutoka pwani ya Ukanda wa Gaza hadi nchini mwake baada ya kuishi katika eneo hilo la Palestina kwa kipindi cha yapata miaka miwili bila hati mwafaka.

Mwanamume huyo Mohamed Salman Omeira Awda alipatikana na polisi wa Misri kwenye eneo lililo na umbali wa kilomita kutoka baharini na kumzuia ili kumhoji.Bwana Awda alieleza kuwa aliingia Ukanda wa Gaza mwezi Septemba mwaka 2005 wakati majeshi ya Israel yalipoondoka kwenye eneo hilo.Kwa muda wa siku chache usimamizi wa eneo la mpakani ulitoweka kati ya Gaza na Misri jambo lililowawezesha watu kuingia maeneo yote bila kizuizi.

Baada ya kuingia Ukanda wa Gaza alishindwa kurudi kwani hakuwa na hati mwafaka za kujitambulisha.