1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Wabunge wajiuzulu kupinga Musharraf kuwania urais

2 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBKt

Kiasi cha wabunge 80 wa upinzani nchini Pakistan wamejiuzulu kutoka katika bunge wakipinga mipango ya Rais Pervez Musharraf kuwania tena urais katika uchaguzi mkuu wa Jumamosi ijayo.

Wabunge hao wamechakua hatua hiyo kupinga uhalali wa Generali Musharraf kuingia katika uchaguzi huo wakati akiwa na cheo cha ukuu wa majeshi wakisema kuwa ni kinyume cha sheria na katiba ya nchi hiyo.

Ijumaa iliyopita mahakama kuu ya Pakistan ilitoa hukumu ya kumruhusu Musharraf kuwania tena urais wakati akiwa na cheo cha ukuu wa majeshi.

Kiongozi huyo wa Pakistan amesema kuwa atajiuzulu cheo cha ukuu wa majeshi kabla ya tarehe 15 mwezi Novemba iwapo atashinda uchaguzi huo.