ISLAMABAD:Uamuzi wa mahakama kuu waendelea kupingwa
30 Septemba 2007Matangazo
Polisi wa kukabiliana na fujo wametumia gesi za kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya wanasheria waliokuwa wakiandamana dhidi ya hatua ya tume ya uchaguzi ya kumuidhinisha rais Pervez Musharraf kugombea tena katika uchaguzi mkuu ujao.Watu kadhaa walijeruhiwa katika mji mkuu Islamabad na Lahore na Karachi.Ghasia zimetokea siku moja baada ya mahakama kuu ya Pakistan kupinga shinikizo kadhaa za kisheria za kutaka kumzuia Musharraf asigombee kipindi kingine cha pili cha urais.Vyama vikuu vya upinzani nchini humo leo hii vimeapa kuanzisha kampeini kali ya kisheria kuishinikiza mahakama kubadili hukumu yake kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 6.