1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Tume ya uchaguzi yabadili sheria,Rais Musharraf habanwi tena

18 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOr

Tume ya uchaguzi nchini Pakistan inatangaza mabadiliko yatakayomuezesha Rais Pervez Musharraf kuwania tena nafasi ya urais bila kujiuzulu kama amiri jeshi mkuu.Vyama vya upinzani vinashtumu hatua hiyo ambayo ni juhudi za kiongozi huyo kubakia madarakani na kuielezea kama ukiukaji wa katiba.

Bwana Musharraf aliingia madarakani mwaka 99 baada ya muongo mmoja wa uongozi wa kiraia uliozongw ana ghasia na kuahidi kumaliza msimamo mkali wa waislamu na kudumisha demokrasia.Hata hivyo Rais Musharraf bado anasubiriwa kutangaza lini atakapojiuzulu kama kiongozi wa jeshi wadhifa unaompa madaraka zaidi.

Uchaguzi wa rais unapangwa kufanyika tarehe 15 mwezi Oktoba.