ISLAMABAD:Mzozo wa Lal Masjid waelekea ukingoni | Habari za Ulimwengu | DW | 11.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD:Mzozo wa Lal Masjid waelekea ukingoni

Hatimaye mzozo wa msikiti mwekundu nchini Pakistan unaelekea kumalizika baada ya wanajeshi waliovamia msikiti huo kumuua kiongozi mwenye itikadi kali aliyekuwa amejificha ndani ya msikiti huo pamoja na wafuasi wake.

Abdul Rashid Ghazi inadaiwa ameuwawa kwenye mapambano ya risasi pamoja na wafuasi wake 50.wanajeshi wanane pia waliuwawa kwenye mapambano hayo. Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya PakistnaJaved Iqbal Cheema wapiganaji walionusurika waliendeleza mapambano hata baada ya kuuwawa kiongozi wao.

Watoto na kina mama waliokuwa wanatumiwa na wanamgambo kama ngao ya kujikinga walifanikiwa kutoroka msikiti huo.

Cheema ametetea uamuzi wa serikali juu ya umwagikaji damu huo akisema ilijaribu kiasi cha kutosha kuutatua mgogoro kupitia mazungumzo lakini Ghazi aliamua kuchukua msimamo mkali na hivyo kusabisha kusambaratika kwa juhudi hizo na kuilazimu serikali kuchukua hatua kali.

Serikali ya mjini Washington pia imetoa taarifa ikisema mshirika wake katika vita dhidi ya Ugaidi rais Pervez Musharaf alichukua jukumu linalostahili ili kuweka amani.Hata hivyo inaahofiwa kwamba huenda kukazuka mashambulio ya kulipiza kisasi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com