1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Islamabad:Kiasi ya watu 51 wauawa katika miripuko Pakistan

Watu wapatao 51 wameuwawa nchini Pakistan katika hujuma tatu tafauti za kujitoa mhanga kwa kujiripua, huku shinikizo likiongezeka dhidi ya Rais Pervez Musharraf baada ya hatua yake kali ya kupambana na wanaharakati wa Kiislamu wiki iliopita. Bomu moja liliripuka katika msikitini katika kambi moja ya kijeshi katika mji wa kaskazini magharibi wa Kohat na kuwauwa watu 15. Mabomu mengine mawili yaliripuaka katika mji wa kusini wa Hub na ule wa kaskazini ya mbali wa Hangu na kuwauwa jumla ya watu 36. Kwa jumla zaidi ya watu 180 wameuwawa tangu majeshi ya usalama yalipouvamia msikiti wa Waislamu wa itikadi kali mjini Islamabad mapema mwezi huu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com