Islamabad.Jeshi la serikali lashambulia eneo la wataliban na kuwauwa. | Habari za Ulimwengu | DW | 30.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Islamabad.Jeshi la serikali lashambulia eneo la wataliban na kuwauwa.

Helikopta za kijeshi za Pakistan zimewauwa watu wanaotuhumiwa kuwa ni wanamgambo 80 katika shambulio lililofanywa katika kambi moja karibu na Khar katika eneo la Bajaur linalopakana na Afghanistan.

Afisa wa jeshi amesema, shambulio la vikosi vya serikali lililenga zaidi madrasa ambayo inakisiwa kukaliwa na wapiganaji 70 hadi 80 karibu na mji wa Khar, mji mkuu wa jimbo la Bajaur.

Mashambulizi hayo yamekuja siku mbili baada ya watu wanaotuhumiwa kuwa Wa-Taliban 5,000 kufanya maandamano katika maeneo ya Bajur karibu na Damadola, katika kijiji ambacho kipo karibu na pahala palipofanywa shambulio na jeshi la Marekani mwezi January na kupelekea kuuwawa kwa wafuasi kadhaa wa Al-Qaida na wananchi wa kawaida.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com