ISLAMABAD:Benazir Bhutto azuiliwa nyumbani mwake | Habari za Ulimwengu | DW | 09.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD:Benazir Bhutto azuiliwa nyumbani mwake

Polisi nchini Pakistan waliojihami kwa magari ya kupambana na ghasia wanazingira nyumba ya Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo Bi Benazir Bhutto.Wafuasi wake 5,000 wanaripotiwa kukamatwa na polisi ili kuzuia mkutano wa hadhara kufanyika ili kupinga hali ya hatari iliyotangazwa mwishoni mwa juma lililopita.Kulingana na uongozi mikutano ya hadhari imepigwa marufuku katika hali ya hatari .Mkutano wa Bi Bhutto ulipangwa kufanyika mjini Rawalpindi hii leo.Kwa mujibu wa meya wa mji huo ripoti ya kuaminika inaeleza kuwa huenda walipuaji wa kujitoa muhanga wanaandaa kushambulia mkutano huo.Rais Musharraf bado anawabana wapinzani wake hata baada ya kutangaza kuwa uchaguzi utafanyika mwezi Februari ikiwa ni mwezi mmoja baada ya tarehe iliyowekwa awali.

''Uchaguzi sharti ufanyike haraka iwezekanavyo kwavile tumeshatathmini hali yote.Uchaguzi lazima ufanyike ifikapo tarehe 15 mwezi februari mwaka ujao ''

Tangazo hilo linatolewa baada ya shinikizo kutoka kwa Marekani iliyo mwandani wake mkuu wa kimataifa.Polisi waliwashambulia wafuasi yapata 300 wa Bi Bhutto walipokusanyika ili kufunga safari ya Rawalpindi na kuwakamata 25.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com