ISLAMABAD. Waziri ajiuzulu kupinga njama ya rais Musharaf kutaka kubakia madarakani | Habari za Ulimwengu | DW | 28.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD. Waziri ajiuzulu kupinga njama ya rais Musharaf kutaka kubakia madarakani

Waziri anayehusika na teknolojia ya habari nchini Pakistan, Ishaq Khan Khakwani, amejiuzulu kupinga mpango wa rais Pervez Musharaf kutaka kuendelea kubakia madarakani.

Waziri huyo amesema anajiuzulu wadhifa wake lakini ataendelea kuwa mtiifu kwa chama tawala cha Paksitan Muslim League Quaid, PML- Q.

Waziri Ishaq ametaka kufanyike mdahalo wa kitaifa utakaovijumulisha vyama vya kisiasa vya upinzani.

Wakati huo huo, mbunge Ali Hassan Gilani, ambaye ni katibu wa bunge anayehusika na maswala ya sayansi na teknolojia, amesema anakihama chama tawala na kujiunga na chama cha waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Nawaz Sharif.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com