1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Watu 80 wauwawa katika mapigano.

8 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Hd

Idadi ya watu waliouwawa katika mapigano makubwa ya siku mbili kati ya jeshi la Pakistan na wapiganaji katika eneo la ukanda wa kikabila katika mpaka na Afghanistan imepanda na kufikia watu 80. Wanajeshi 20 wa jeshi la Pakistan pia wameuwawa katika mapigano hayo, ambayo yalitokea katika jimbo linalounga mkono wapiganaji wa Taliban karibu na mpaka na Afghanistan. Majeshi yakisaidiwa na helikopta yalifanya mashambulizi kusini mwa mji wa Mir Ali kaskazini mwa jimbo la Waziristan jana Jumapili kufuatia mashambulizi ya wapiganaji dhidi ya mlolongo wa magari ya jeshi.

Wakati huo huo raia wanane, ikiwa ni pamoja na wanawake watano, wameuwawa na wengine saba wamejeruhiwa wakati nyumba katika mji wa Mir Ali ziliposhambuliwa kimakosa na majeshi ya Pakistan.

Wakati huo huo wanajeshi wanne wameuwawa wakati helikopta ilipoanguka wakati wa ziara ya rais Pervez Musharraf katika jimbo la Kashmir leo wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya mwaka wa pili baada ya kutokea tetemeko kubwa la ardhi. Rais Musharraf ambaye alizoa kura nyingi katika uchaguzi wa Jumamosi alikuwa katika helikopta nyingine.