ISLAMABAD: Wapinzani wa Musharraf watawanywa kwa nguvu
29 Septemba 2007Matangazo
Polisi nchini Pakistan wametumia nguvu kuvunja maandamano dhidi ya Rais Pervez Musharraf.Vikosi vya kulinda usalama,vimetumia marungu na gesi ya kutoa machozi,kutawanya makundi ya upinzani.Raia na wanasheria wanapinga kiongozi wa kijeshi Pervez Musharraf kugombea awamu nyingine. Halamashauri ya Uchaguzi lakini imethibitisha kuwa Musharraf atagombea uchaguzi wa rais uliopangwa kufanywa tarehe 6 Oktoba.