1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD : Wapinga kuondolewa kwa hakimu mkuu

13 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAK

Waandamanaji wamelitia moto sanamu la Rais Pervez Musharraf wa Pakistan leo hii na kutowa wito wa kujiuzulu kwake wakati maelfu walipoandamana wakati wa kusikilizwa mahkamani kwa kesi ya hakimu mkuu wa nchi hiyo aliondolewa madarakani na serikali.

Musharraf alimsitisha kazi Iftikhar Choudhury kwenye wadhifa wake wa hakimu wa Mahkama Kuu mwezi uliopita ili kuwezesha jopo la mahakimu kuchunguza tuhuma kwamba alikuwa akitumia vibaya madaraka yake ambapo wakati mmoja inadaiwa kuwa alikuwa akitaka kupandishwa cheo kwa mtoto wake wa kiume.

Lakini watu wanaomkosowa Musharraf wanamshutumu Generali huyo kwa kudhoofisha uhuru wa vyombo vya mahkama na kujaribu kumn’goa hakimu huyo mwenye msimamo thabiti kabla ya uchaguzi wa nchi hiyo ambao unaweza kuchochea changamoto za kisheria dhidi ya kuendelea kwa utawala wake.