1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Soomro kuongoza serikali ya mpito Pakistan

16 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CImT

Rais wa Pakistan,Jemadari Pervez Musharraf amemuapisha waziri mkuu wa mpito kuiongoza nchi hadi uchaguzi wa Januari ijayo.Mwenyekiti wa Bunge,Mohammadmian Soomro alie na umri wa miaka 57,ameapishwa katika kasri la rais mjini Islamabad.Musharraf amesema,Pakistan sasa ipo njiani kuelekea demokrasia.

Hapo kabla,serikali ilimuachia huru kiongozi wa upinzani Benazir Bhutto,aliekuwa katika kizuizi cha nyumbani.Hata hivyo,serikali imesema,polisi watabakia nje ya nyumba ya Bhutto mjini Lahore kwa sababu za usalama.

Kwa upande mwingine,Naibu Waziri wa Nje wa Marekani,John Negroponte anatazamiwa nchini Pakistan ambako atakutana na Rais Musharraf na kumshinikiza kuiondosha hali ya hatari aliyotngaza Novemba 3.