1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD : Sheik Ghazi auwawa

Sheikh mkuu wa Msikiti Mwekundu ameuwawa leo hii wakati wanajeshi wa Pakistan wakiwachomowa wanamgambo waliojichimbia kwenye chuo cha kidini cha wanawake katika mapigano ya chumba hadi chumba.

Kwa mujibu wa msemaji wa serikali sheikh huyo wa itikadi kali Abdul Rashi Ghazi ameuwawa katika shambulio hilo la serikali na kwamba mwili wake ulipatikana kwenye chumba cha chini ya ardhi katika chuo hicho.

Katika mapigano ya kuuvamia msikiti huo katika mji mkuu wa Islamabad takriban wanamgambo 50 wameuwawa pamoja na wanajeshi wanane wa serikali wakati wanajeshi wengine 29 wamejeruhiwa.

Awali msemaji wa jeshi Meja Generali Waheed Arshad amesema mchakato wa uvamizi wa msikiti huo ulikuwa ni wa hatua kwa hatua ili kuepuka maafa na uharibifu usio wa lazima.

Habari za hivi punde tu zinasema kwamba takriban eneo zima la msikiti huo sasa liko mikononi mwa wanajeshi wa serikali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com