1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Shambulizi la kujitolea muhanga limeua watu 6

18 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhX

Polisi nchini Pakistan imeimarisha ulinzi wa usalama katika mji mkuu Islamabad,huku idadi ya watu waliouawa katika shambulio la kujitolea muhanga ikifikia 16.Zaidi ya 60 walijeruhiwa katika shambulio hilo la bomu lililofanywa nje ya mahakama,ambako Mwanasheria Mkuu Iftikhar Chaudhry alieachishwa kazi,alitazamia kutoa hotuba.Wakati wa shambulizo hilo,Chaudhry ambae sasa amekuwa ishara ya upinzani dhidi ya utawala wa miaka minane wa Rais Pervez Musharaff,alikuwa bado hajawasili.Bomu jingine lililoripuka kando ya barabara,karibu na magari ya kijeshi na raia katika eneo la mpakani na Afghanistan,limejeruhi watu wasiopungua saba.Mashambulizi ya aina hiyo yameongezeka nchini Pakistan,tangu vikosi vya serikali kuuvamia Msikiti Mwekundu mjini Islamabad na kuua wafuasi wa itikadi kali.