ISLAMABAD: Pakistan yaadhimisha miaka 60 ya uhuru | Habari za Ulimwengu | DW | 14.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Pakistan yaadhimisha miaka 60 ya uhuru

Pakistan inaadhimisha miaka 60 ya uhuru kutoka kwa Uingereza hii leo. Sherehe za maadhimisho zinafanywa kukumbuka kugawanyika kwa bara hilo dogo mnamo mwaka wa 1947 katika sehemu mbili, Pakistan yenye idadi kubwa ya waislamu na India iliyo na idadi kubwa ya Wahindi.

Watu wamenyaa kimya kwa dakika moja kukumbuka maelfu ya watu waliouwawa kwenye maandamano yaliyotokea wakati huo.

Katika ujumbe wake wa siku ya uhuru rais wa Pakistan, Pervez Musharaf, amewashawishi Wapakistan wawaunge mkono wabunge wasio na msimamo mkali wa kidini kwenye uchaguzi wa bunge unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Utawala wa rais Musharaf unakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wanamgambo wa kiislamu. Nchi jirani ya India itasherehekea uhuru wake hapo kesho.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com