1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Pakistan imejaribu kombora la masafa mafupi

3 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMt

Pakistan imesema,imejaribu kombora la masafa mafupi,ambalo huweza kupachikwa bomu la atomu.Kwa mujibu wa jeshi la Pakistan,jaribio la kombora hilo limefanikiwa,lakini hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.Tarehe 23 mwezi Februari,Pakistan iliripoti kufanya jaribio la kombora la masafa marefu kwa mafanikio.Siku mbili kabla,Pakistan na India zilitia saini makubaliano ya kupunguza hatari ya kutokea ajali za silaha za nyuklia.