ISLAMABAD: Pakistan imejaribu kombora jipya
25 Agosti 2007Matangazo
Pakistan imefanikiwa kufanya jeribio la kombora jipya la kupiga doria angani,ambalo huweza kupachikwa silaha za nyuklia.Kombora Ra’ad lililojengwa nchini Pakistan,linaweza kurushwa na ndege kutoka angani na kwenda umbali wa kilomita 350.
Rais Pervez Musharraf na Waziri Mkuu Shaukat Aziz wamewapongeza wanasayansi na wahandisi waliofanya kazi pamoja kuunda kombora hilo jipya.