1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Mashambulizi ya bomu Pakistan yameua watu 34

19 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBh2

Mashambulizi mawili ya kujitolea maisha muhanga, yameua si chini ya watu 34 nchini Pakistan,huku machafuko ya kuipinga serikali ya Rais Pervez Musharaff yakiendelea.

Watu 29 waliuawa katika shambulio lililofanywa mji wa Hub kwenye Wilaya ya Baluchistan,kusini-magharibi mwa nchi. Mshambuliaji aliejitolea muhanga,alibamiza gari lake lililopakiwa miripuko,katika msafara wa wafanyakazi wa Kichina,waliokuwa wakisindikizwa uwanja wa ndege wa Karachi.

Hapo awali,hadi watu sita waliuawa katika shambulizi lililolenga taasisi ya polisi.Zaidi ya watu 150 wameuawa katika wimbi la mashambulizi,tangu vikosi vya serikali kuvamia Msikiti Mwekundu mjini Islamabad,juma lililopita.