1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Kiongozi awataka wafuasi wake wajisalimishe

Kiongozi aliyekamatwa wa msikiti wenye msimamo mkali uliozingirwa na polisi katika mji mkuu wa Islamabad nchini Pakistan amewataka wafuasi wake wajisalimishe kwa polisi.

Abdul Aziz ameviambia vyombo vya habari vya Pakistan kwamba wanafunzi kadhaa bado wamo ndani ya Masjid Lal na wengine wakiwa na silaha.

Takriban wanafunzi 50 wameondoka kutoka kwenye msikiti huo leo hii.

Mapema leo polisi walitegua vifaa vya kulipuka nje ya msikiti huo na baadae polisi walilazimika kujibu mashambulio ya risasi.

Watu wapatao 16 wameuwawa kufuatia vurugu za siku mbili.

Masjid Lal au msikiti mwekundu unahusika na kampeni zinazoitaka serikali ya Pakistan iidhinishe baadhi ya sharia za kiislamu katika katiba ya nchi hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com