ISLAMABAD. Kiapo kutokomeza itikadi kali Pakistan
13 Julai 2007Matangazo
Rais Pervez Musharraf wa Pakistan,amekula kiapo kutokomeza itikadi kali nchini mwake.Amesema hayo kwenye televisheni,kufuatia kumalizika kwa mapambano ya siku nane kwenye Msikiti Mwekundu wa mjini Islamabad.Watu wasiopungua 105 waliuawa katika mapambano hayo.Wengi waliouawa,walikuwa wanamgambo na walizikwa haraka haraka,alfajiri ya siku ya Alkhamisi,kwenye makaburi yasio na majina.Wakati huo huo,kwenye ukanda wa video, naibu kiongozi wa Al-Qaeda,Ayman al-Zawahiri ametoa wito wa kulipiza kisasi.