Ireland kufuta marufuku ya utoaji mimba
26 Mei 2018Kura hiyo iliyopigwa kwa minajili ya kuondoa marufuku iliyomokwa mujibu wa uchunguzi wa maoni katika kura ya maoni ya kihistoria katika nchi hiyo ambayo kimsingi ina Wakatoliki wengi. katika katiba ya kutoa mimba isipokuwa tu katika wakati ambapo maisha ya mama yamo hatarini ilitarajiwa kushinda kwa wingi wa theluthi mbili ya kura.
Uchunguzi wa maoni uliofanywa na gazeti la Irish Times umeonesha kwamba asilimia 68 ya Waireland walipiga kura ya "ndio" kufanya mabadiliko ya nane ya katiba, wakati uchunguzi wa maoni uliofanywa na kituo cha televisheni ya taifa RTE kimeweka idadi ya wanaokubali kuwa asilimia 69.4.
Taasisi ya uchunguzi wa maoni ya Ipsos/MRBI iliwauliza zaidi ya wapiga kura 4,500 katika maeneo 160 ya kupigia kura katika kila jimbo la uchaguzi kwa ajili ya gazeti la Irish Times, kukiwa na uwezekano wa makosa unaokaribiwa kuwa asilimia 1.5.
Uchunguzi wa RTE ulihusisha watu 3,800 na ukiwa na wastani wa makosa wa asilimia 1.6.
Umeonesha mgawanyiko mkubwa miongoni mwa makundi ya umri , ambapo asilimia 87.6 ya watu wenye umri kati ya miaka 18-24 wakipiga kura ya "Ndio" wakati watu wenye umri wa miaka 65 na kuendelea ni kundi pekee lililokataa mabadiliko, ambapo asilimia 58.7 walipiga kura ya "Hapana".
Watu waliojitokeza kupiga kura walikuwa wengi ambapo katika baadhi ya maeneo kumeripotiwa idadi ya zaidi ya asilimia 70, kwa mujibu wa RTE.
"Inaonekana kuwa tutaandika historia kesho," waziri mkuu Leo Varadkar , ambaye amefanya kampeni ya "Ndio" , aliandika katika ukurasa wa Twitter. Matokeo rasmi hayatarajiwi hadi leo Jumamosi mchana. Kura hiyo imeligawa taifa hilo ambalo kimsingi lina waumini wengi wa Kikatoliki, huku kukiwa na hisia kali katika pande zote zilizoshiriki katika mjadala huo.
Maisha ya mama pia ni muhimu
Utoaji mimba unaruhusiwa tu kwa sasa iwapo maisha ya mama yamo hatarini lakini sio katika matukio ya kubakwa ama udhalilishaji kingono kupitia ndugu.
Kiongozi wa upinzani wa chama cha Sinn Fein Mary Lou McDonald, ambaye pia alifanya kampeni ya "Ndio" , ameieleza kura hiyo ya maoni kuwa ni "kufunga ahadi na hatma kwa sisi wote" wakati akipiga kura yake mjini Dublin.
Kura hiyo ilifuatia miezi kadhaa ya mjadala mkali baina ya wale wanaofanya kampeni ya kura ya "Ndio" na "Hapana" juu ya iwapo nchi hiyo ifanye mabadiliko yake ya nane ya katiba, ambayo inampa mama na mtoto ambaye bado hajazaliwa " haki sawa ya kuishi" iwapo itabadilishwa.
Wapiga kura waliulizwa iwapo wanataka kuendelea na sheria hiyo ama kuibadilisha, ambapo iwapo itabadilishwa kutaongezwa kipengee kipya katika katiba ambacho kitatoa uwezo kwa bunge kuhalalisha utoaji mimba.
Waliokuwa wanafanya kampeni ya "Ndio" wanadai kwamba kifungu hicho cha sheria kiliwazuwia madaktari kufanya utoaji mimba hata wakati maisha ya mama yalikuwa hatarini.
Zaidi ya watu milioni 3.2 waliandikishwa kupiga kura katika kura hiyo ya maoni , ambayo inafuatia miito ya mara kwa mara kutoka Umoja wa mataifa kuifanyia mabadiliko sheria hiyo nchini Ireland na kuwa katika mstari mmoja na viwango vya sheria za kimataifa za haki za binadamu.
Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae
Mhariri: Caro Robi